Dukani - Simamia biashara yako was an overall app developed by KAPPU FINTECH LIMITED. It was removed from Google Play Aug 18, 2026 and is no longer available for download.
Download Statistics
User Ratings
The app had no ratings.
App Information
Dukani - Simamia biashara yako was free to download. The APK download size was 48.48 MB. The last available version was 3.0.1. The last update was on August 14, 2026.
Technical Requirements
The app had a content rating of Everyone. The app had been available on Google Play May 2026.
Description
Dukani — Simamia biashara yako kwa uelewa zaidi
Dukani ni programu rahisi na salama ya kusimamia biashara, iliyoundwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wa kati Tanzania.
Iwe una duka la rejareja, grocery, kiosk, minimarket, jumla au biashara nyingine, Dukani inakusaidia kurekodi na kufuatilia shughuli muhimu za biashara yako kwa urahisi.
Jua mauzo yako, fuatilia bidhaa zako, simamia madeni na gharama, na pata picha nzuri ya biashara yako — hata ukiwa huna intaneti.
SIMAMIA BIASHARA YAKO
Dukani inakusaidia:
• Kurekodi mauzo kwa haraka • Kufuatilia bidhaa na stock • Kurekodi manunuzi na kuongeza stock • Kufuatilia wateja na wauzaji • Kusimamia mauzo ya mkopo na madeni • Kurekodi gharama za biashara • Kufuatilia bei ya kununua na kuuza • Kuona taarifa na ripoti za biashara yako
Fuatilia STOCK kwa urahisi
Jua bidhaa ulizonazo na jinsi stock yako inavyobadilika kutokana na mauzo, manunuzi na marekebisho.
Dukani pia inakusaidia kutumia vipimo tofauti kama: - Kipande - Box - Dozen - Kg - Lita na vipimo vingine kulingana na biashara yako.
ELEWA MAUZO NA FAIDA YAKO
Usiishie kujua umeuza kiasi gani.
Dukani hukusaidia kupata picha ya biashara yako kwa kutumia taarifa za mauzo, gharama na bidhaa zako.
Jua biashara yako vizuri zaidi na fanya maamuzi ukiwa na taarifa sahihi.
BIASHARA YENYE WAFANYAKAZI?
- Dukani inaweza kusaidia biashara yenye wafanyakazi kusimamia shughuli za kila siku huku mmiliki akiwa na uelewa wa kinachoendelea kwenye biashara. - Mmiliki anaweza kufuatilia shughuli za biashara bila kutegemea taarifa za maneno pekee.
INAFANYA KAZI HATA BILA INTANETI
- Huna internet muda wote? Hakuna tatizo. - Dukani imeundwa kufanya kazi hata wakati hakuna muunganisho wa internet. Unaweza kuendelea kurekodi mauzo na kusimamia taarifa za biashara yako. - Internet inapopatikana, taarifa husawazishwa na mfumo kulingana na utaratibu wa Dukani.
TAARIFA ZA BIASHARA YAKO
- Taarifa za biashara yako huhifadhiwa kwenye kifaa chako na kusawazishwa na mfumo unapopatikana mtandao. - Hii inakusaidia kuendelea kufanya kazi hata maeneo yenye internet hafifu au isiyotabirika.
IMETENGENEZWA KWA MAHITAJI YA BIASHARA ZA TANZANIA
Dukani imejengwa kwa kuzingatia mazingira halisi ya biashara — kuanzia maduka madogo hadi biashara zinazokua.
Lengo ni moja:
Kukusaidia kuelewa biashara yako, kuisimamia vizuri na kufanya maamuzi bora.
ANZA LEO
Pakua Dukani, ongeza bidhaa zako na anza kurekodi biashara yako.
Each subscription will automatically renew 3 days before the expiration date for
the same time period. Subscriptions can be cancelled at any time before the renewal.